Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Said Mtanda akiwa ameambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, Mkuu wa Magereza Mwanza, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Maofisa, Wakaguzi na Askaria wa R&F kutoka vyombo vya usalama, Familia pamoja na wananchi kuaga mwili wa X.F.7768 CPL Tumsifu Wilson Kileo.
Akizungumza katika ibada ya kuaga mwili iliyofanyika leo Februari 16.2026 huko nyumbani kwake Mtaa wa Kagera, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Said Mtanda amesema, maisha ni kama hadithi na tuwe na hadithi nzuri zitakazosimuliwa kwa mujibu wa matendo yetu, kwani kwa wale ambao wamepata nafasi ya kuwatumikia wananchi tunatakiwa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ili kuhakikisha hadithi yetu inakuwa nzuri pindi itakaposimuliwa mwisho wa uhai wetu.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa ametoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa familia, ndugu na jamaa kwa kupoteza mpendwa wao na Askari kwa kupoteza mpiganaji mahiri ambaye alikuwa ni mtu wa watu na aliyependa kushirikiana na Askari wenziwe pamoja na wananchi, jambo lililomfanya aheshimiwe na wengi enzi za uhai wake.
Aidha, amewaahidi familia ya marehemu kuwa nao bega kwa bega katika kipindi hiki chote cha msiba mpaka mwili utakapo pumzishwa katika nyumba yake ya milele na wasisite kutoa taarifa pindi wanapohitaji msaada kutoka Jeshi la Polisi kwani lipo tayari kuwasaidia kipindi chote.
Ibada ya kuuaga mwili wa X.F7768 CPL Tumsifu Wilson Kileo, uliongozwa na Mchungaji Kiongozi Usharika wa Gali laya Buhongwa, kutoka Kanisa Katoliki la Galilaya Buhongwa.
Marehemu alifariki Tarehe 13.2026 majira ya 08.30 Mchana katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kulazwa, Tarehe 10/2/2026 wakati alipopata ajali ya kugongwa na gari akiwa kazini. mwili unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Kijiji cha Liamungu, Mkoa wa Kilimanjao kwa ajili wa kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele.













