BODABODA 500 mbioni kufanya kazi UAE

GEORGE MARATO TV
0


Serikali imeendelea kufungua fursa za Ajira nje ya nchi , ambapo Vijana kutoka sehemu mbalimbali wamejitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kushiriki zoezi la usajili wa madereva bodaboda 500 wanaotarajiwa kwenda kufanya kazi katika Nchi za Falme za Kiarabu (UAE).

Zoezi hili ni sehemu ya muendelezo wa utekelezaji wa programu ya Serikali ya kuwaunganisha watanzania na fursa za Ajira nje ya Nchi kupitia Mifumo rasmi ili kuhakikisha ulinzi wa haki na usalama wao. 

Akizungumza leo Februari 10, 2026 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Jane Sorogo amesema kuwa vijana wamejitokeza kwa wingi katika usaili wa mahojiano ambapo baada ya Dar es Salaam usaili utafanyika katika Mkoa wa Tanga na Mwanza.



"Vijana watakaofaulu usaili huo wataelekea katika kituo cha Kazi Nchini Falme za Kiarabu (UAE) Pia Nawasihi vijana kuchangamkia fursa za ajira za nje ya nchi zinazojitokeza, kwani  ni fursa ambazo nyuma yake kuna serikali.". Amesema Sorogo.

Wakizungumza kwa wakati tofauti wanufaika wa ajira hiyo ya nje ya nchi wameishukuru Serikali kwa fursa za ajira nje ya nchi kwa vijana wa kitanzania, aidha wameiomba Serikali kutowaacha kuendelea kuwasimamia wanapokuwa nje ya Nchi huku wakiwasihi vijana wenzao kukimbilia fursa hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top