WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 18, 2025 amekagua Jengo la Ofisi ya Kituo cha Forodha kwa Pamoja-Kasumulu ambacho kiliathiriwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya umma na mali za watu binafsi zilizoathiriwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29 Mwaka huu nchini.






