MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara mh Agnes Mathew Marwa amekabidhi mchango wa saruji na mchanga kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa ofisi ya mtendaji wa kata ya Bweri katika halmashauri ya Manisipaa ya Musoma mkoani Mara.
Mchango huo umekabidhiwa na diwani wa viti maalum katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mh Sister Yohana kwa niaba ya mbunge Agness Marwa katika kikao cha kwanza cha maendeleo cha kata ya Bweri chini ya uenyekiti wa diwani wa kata hiyo Paul Katikiro.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko mitano ya saruji na mchanga kwa ujenzi wa ofisi hiyo hiyo inayotumiwa pia na diwani wa kata ya Bweri,Mh Sister Yohana,amesema mbunge Agness kama kada wa CCM, ametoa mchango huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kazi kubwa inafanywa na watendaji wa serikali pia itamwezesha diwani kupata sehemu nzuri ya kufanyia kazi katika kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabioi wananchi wa kata yake
Amesema kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara anayetokana na CCM, ataendelea kusaidia ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Sister Yohana amewataka watendaji wa mitaa kata pamoja na wenyeviti katika kata hiyo kufanya kazi Kwa kushirikiana Ili kuleta Maendeleo ya haraka yanayotarajiwa na wananchi wa kata ya Bweri.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo,diwani Katikiro amempongeza mbunge Agness kwa kujali na kutoa mchango wa ujenzi wa ofisi hizo huku akitoa ahadi ya kumpa kila ushirikiano katika kuisaidia kata hiyo.







