MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara mh Agnes Mathew Marwa amekabidhi mchongo wa saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama cha Mapinduzi kata ya Bweri katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mchango huo umekabidhiwa na diwani wa viti maalum katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mh Sister Yohana kwa niaba ya mbunge Agness Marwa katika kikao cha kwanza cha maendeleo cĥa kata ya Bweri chini ya uenyekiti wa diwani wa kata hiyo Paul Katikiro.
Akuzungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji na mchanga kwa ujenzi wa ofisi hiyo ya CCM kata ya Bweri,Mh Sister Yohana, amesema mbunge Agness kama kada wa CCM, ametoa mchango huo katika sehemu ya kuunganisha kazi kubwa inafanywa na viongozi wa CCM katika kuisimamia Serikali yake.
Amesema kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara anayetokana na CCM, ataendelea kusaidia ujenzi wa ofisi za chama na miradi mingine ya Maendeleo katika kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha amewataka watendaji wa mitaa pamoja na wenyeviti katika kata hiyo kufanya kazi Kwa kuleta Ili kuleta Maendeleo ya haraka yanayotarajiwa na wananchi wa kata ya Bweri.
Sauti baada ya kupokea msaada huo,diwani Katikiro amepongeza mbunge kwa kujali na kutoa mchango wa kuimarisha chama cha mapinduzi hukukitoa ahadi ya kumpa kila wakati katika kuisaidia kata hiyo.








