Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ametembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita.
Katika ziara hiyo, Mhe. Majaliwa amepata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.