Peter Zakaria Ateuliwa Chifu wa 7 Kabila la Kurya Koo ya Butimbaru

GEORGE MARATO TV
0

Mdau wa maendeleo mkoa wa mara na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Ndg. Peter Zakaria leo Tarehe 24 September 2025 amepokea wito wa kufika katika kilinge/baraza/eneo wanapokalia wazee wa mila ya koo ya Butimbaru Inchage linaloitwa "Kungurutani" linalopatikana katika kijiji cha mogabiri ikiwa ndio eneo linalotumika kutatua migogoro inayofikishwa na jamii ya kurya ndani ya hilo la mila.

Zakaria alifika na kupashwa habari ya Uteuzi wa jina lake kupendekezwa kati ya majina mengi na kuibuka kidedea kuwa chief wa koo hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho cha mila mwenyekiti wa mila koo ya butimbaru na mjumbe wa koo 12 Ndg.Charles Mwita Mgogo amesema wazee wamemteua kuwa chifu wao baada ya kufanyika kwa vikao mbalimbali vya majadiliano na wito huo wa leo kwa Zakaria ni kwaajili ya kupashwa habari hiyo ili kujua utayari wake.

"Hapa tulipo ndio makao yetu tunapokalia kwaajili ya kutatua migogoro ya wananchi pamoja na kumsikiliza shida zao mbalimbali. Leo imekuwa ni siku nzuri na maalumu ya kukutana na mteule wetu ambaye imewapendeza wazee kumchagua Zakaria kuwa chifu wetu" Charles M. Mgogo

Naye kwa upande wake Ndg. Peter Zakaria amesema taarifa hizo zimekuwa za ghafla na nzuri sana kwake na kwa familia yake pia maana anafahamu koo hiyo ina wazee wengi sana lakini imewapendeza kumchagua yeye.

"Mimi nimefurahi sana hata watoto wangu waliposikia napewa UCHIFU walifurahi wakasema wazee hawa wamefikiria nini baba mpaka waje wakuteue wewe na kuna wazee wengi. nikawaambia hao wazee ni wenzangu sasa na niko tayari na nimejitolea" Peter Zakaria 

Aidha Charles Mgogo amesema maandalizi ya kumsimika (Uapisho) wa chifu Zakaria kuanza mara moja na sherehe hizo kutarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top