Mwenge wa Uhuru Kupitia Miradi ya Bilioni 23.8 Mkoani Kagera

GEORGE MARATO TV
0


 Angela Sebastian; Muleba

Jumla ya Miradi ya Maendeleo 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 23.8 itazinduliwa , Kukaguliwa , kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Kagera.

Akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigella leo Septemba saba katika kata ya Nyakabango, mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa alisema, kuwa kwa mwaka 2024 Mwenge wa Uhuru ulitembelea, kukagua,Kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye Jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi bilioni 53.9

Hajat Mwassa alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Kagera utakimbizwa katika halmashauri zote 8 za mkoa huo kwa umbali wa kilometa 1,040.

Wakati huo huo Mwassa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo katika Sekta mbalimbali mkoani humo kwani, miradi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali, Wananchi pamoja na wadau wa maendeleo .

Aidha amesema kwa kuzingatia ujumbe wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 ambao ni "Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu" mkoa wa Kagera umetekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

 Aidha amewashauri wananchi na vyama vya siasa pamoja na makundi yote wakiwemo Vijana, Wazee na watu wenye mahitaji maalum kushiriki uchaguzi mkuu utakao fanyika October 2025 ili kutimiza haki yao ya kikatiba 

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi wa Barabara ya Katembe - Mwaloni yenye urefu wa Kilometa 0.56 kwa kiwango cha Lami amesema, kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni kutokana na dhamira na maono ya Dk.Rais .

Aidha ameongeza kuwa Tanzania inayo Tunu ya Taifa ambayo Mwananchi yoyote akiiona anajua kuwa mahali hapo Tunu inaenda kuweka matumaini , Upendo na heshima katika maeneo hayo kwani ipo miradi ambayo watu walidhani haiwezi kutekelezwa lakini Mwenge wa Uhuru umeizindua.


 Pia amewaomba wananchi kuitunza miradi hiyo ikiwemo Barabara na kuendelea kuithamini kwa dhati .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top