Chatanda: CCM imetuheshimisha wanawake, UWT tunatafuta kura za kishindo za Dk. Samia

GEORGE MARATO TV
0


Na: Mwandishi Wetu, TEMEKE

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda, amesema UWT inashukuru sana maamuzi yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani hiyo inadhihirisha imani kubwa ya Chama kwa wanawake katika nafasi za uongozi.

Chatanda ameyasema hayo Septemba 28, 2025, aliposhiriki Mkutano wa Mgombea Mwenza wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam ambapo amesema wanawake wana uwezo mkubwa wa kiongozi na kiutendaji na Dkt Samia Suluhu Hassan ni amethibitisha hili na ni kielelezo kizuri.

"Ndugu Mgombea Mwenza (Balozi Dkt. Nchimbi), naomba niwaambie wananchi hawa wa Temeke, kwa sisi UWT, Umoja wa Wanawake Tanzania tunaendelea kuwashukuru Chama chetu kwa namna kilivyotuheshimisha sisi wanawake, Chama hiki kimeteua Mgombea Urais mwanamke, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi hii ya Tanzania imeumbwa, imetokea sasa, kwahiyo wanawake wa nchi hii tuna kila sababu ya kuinuka kwenda kumsemea mwanamke mwenzetu, kwenda kumtafutia kura ,tumeshakubaliana makundi yote kwenda kutafuta kura za heshima," amesema Chatanda.

Katika hatua nyingine, Chatanda amemuomba Balozi Dkt. Nchimbi kufikisha salamu za UWT kwa Dkt. Samia kuwa UWT na wanawake kwa ujumla watamchagua kwa kura za mafuriko na za heshima ili aendelee kuwaongoza Watanzania.

Sambamba na hilo, Chatanda amewambea kura wagombea ubunge na udiwani watokanao na CCM ili kuendeleza gurudumu la maendeleo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top