Wasira: Kunung'unika, Kufikisha Ujumbe Kwa Maandamano Hakuleti Chakula.

GEORGE MARATO TV
0


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kunung'unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali kwa njia ya maandamano kumepitwa na wakati.

Amesema Watanzania wanataka maendeleo ukiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na ajira kwa wananchi.

Wasira amesema hayo leo Septemba 28, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, mjini Moshi.

"Wewe unanung'unika tu maandamano utakula maandamano, tunataka reli ya kisasa kwa sababu katika dunia inayoendelea tofauti ya nchi zetu na nchi zilizoendelea ni miundombinu, ukifika tu unaiona barabara pana, kuna reli inakwenda 'speed' kwa hiyo barabara inakwenda speed.

"Hakuna biashara ya kisasa ya kutunza vitu kwa matenga umebeba kichwani, hiyo ni biashara ya zamani, biashara ya kisasa ni ile inayokwenda 'very fast' and speed (inayolwenda haraka).

Kwa mujibu wa Wasira,  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 inaelekeza reli kuunganisha Pugu (Dar es Salaam), Tanga na Arusha kupitia Mkoa wa Kilimanjaro.

"Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka reli iunganishe Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro, na sisi Musoma kule hata isipokuja miaka mitano hii inayokuja mpaka Arusha tunaisubiri na ili tuipate tutahakikisha CCM inaendelea kushinda.

"Ilani inasema sasa Musoma tujenge bandari kama hatua ya kwanza ya kupokea reli na reli ikifika itakuwa inatokea Arusha inatuunganisha na Tanga na sisi tutafanya biashara kati ya Musoma na Port bell ya Uganda," amesema.

Amebainisha kuwa, kwa namna hiyo vijana watapata kazi kwenye reli na kwamba ni muhimu kutafuta majibu ya matatizo mapya mara kwa mara.

Amesisitiza Wasira: Kunung'unika, Kufikisha Ujumbe Kwa Maandamano Hakuleti Chakula.*, zipo njia sahihi na bora zaidi kufikisha ujumbe mahali husika hususan kwa njia ya amani.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top