*Musoma Mjini, Mara – 19 Septemba 2025*
Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Agnes Marwa, leo amefanya ziara ya nyumba kwa nyumba katika Kata ya Mshikamano, Musoma Mjini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushawishi wa CCM kuelekea uchaguzi Mkuu.
Katika ziara hiyo, amekuwa akitafuta kura kwa ajili ya Mgombea wa Urais kupitia CCM, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Ndg. Mgore Miraji Kigera, na Mgombea Udiwani wa Kata ya Mshikamano, Ndg Njofu Constantine Katama.
Ziara hiyo ni maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za udiwani kwa Kata ya Mshikamano, ambapo Agnes Marwa anatarajiwa kuwa *mgeni rasmi*.
“Tunawaeleza wananchi moja kwa moja, kutoka nyumba kwa nyumba, kuhusu umuhimu wa kuendeleza kasi ya maendeleo tuliyonayo chini ya uongozi wa CCM. Ushindi wa mafiga matatu — Rais, Mbunge na Diwani — ndiyo njia pekee ya kuendeleza mafanikio,” alisema Agnes Marwa.