Waziri Mavunde awasili wilayani Namtumbo maandalizi ya ziara ya Rais Samia

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde leo amewasili Wilaya ya Namtumbo,Mkoani Ruvuma kwa ajili ya ukaguzi wa maandalizi ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwenye mradi wa madini ya Urani unaotekelezwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd.





Tarehe 30.07.2025 Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan atazindua Kiwanda cha Uchenjuaji madini ya Urani na pia atazindua rasmi kuanza kwa ujenzi wa mgodi wa Urani na ujenzi wa Mtambo mkubwa wa kuchenjua madini ya Urani ambao unakadiriwa kuwa gharama ya zaidi ya Tsh 3.06 Trilioni.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top