Devotha Daniel Mburarugaba na Samira Khalfani Amour wameibuka washindi kati ya wagombea nane walioshiriki katika uchaguzi wa kura za maoni nafasi ya ubunge wa viti maaluma mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa wanawake Tanzania (UWT).
Akitangaza matokeo hayo,Msimamizi wa Uchaguzi huo mjumbe wa baraza kuu UWT Taifa Yasmin Bachu amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na wagombea nane, jumla ya wapiga kura walikuwa 1,483 ambapo kura moja ilihalibika hivyo kura halili zikiwa 1,482.
Bachu amewataja Devotha Daniel aliyepata kura 1,308 na Samira Khalfani 1,250 kuwa wameongoza katika uchaguzi huo wakifuatiwa na Anitha Korongo kura 153,Elizabeth Ngaiza kura 94,Anitha Bunono kura 52,Anitha Nyamzinga kura 44,Herieth Lugaju kura 37 na Evastina Godian kura 26.
Aidha Bachu amewashauri wajumbe wa UWT mkoa wa Kagera kuwa wakati wa kampuni za Dk.Samia Suluhu Hassan wapaze sauti kwa na kuunganisha nguvu za kumuombea kura zitoshe pia kushinda majinbo yote rb ya mkoa wa Kagera ili kuwawezesha washindi hao wili kuingia bungeni.
Nao wagombea wamesema uchaguzi uliandaliwa kwa mazingira safi na salama wa hali ya juu na kuwaomba wenzao ambao kura hazikutosha kuendelea kuungana na waliochaguliwa kufanya kazi pamoja kwani wote ni wana chama wa chama cha Mapinduzi.
Devotha Daniel amewaomba wajumbe kuungana na kuondoa makundi kwani uchaguzi huo umepita wawe kitu kimoja wote walikuwa wazuri sasa wanajenga nyumba moja hivyo, itasaidia waweze kutafuta kura za Dk.Samia na majimbo yote nane kwa urahisi kwani ndilo jambo kubwa lililopo mbele yao kwasasa.
Kwa upande wa Samira Khalfani ameshukuru kamati ya CCM Taifa kirudisha jina lake na kumuona anafaa katika nafasi hiyo pia,akawaasa wagombea wenzake ambao hawakufanikiwa kupata ushindi wasikate tamaa maana kwenye chama hicho zipo nafasi nyingi hivyo zinapotokea wasiache kugombea maana wote wanahitaji kutafuta kura usiku na mchana ili CCM ishinde.
Naye Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kagera Hajat Faidhah Kainamula amesema katika zoezi la kupata mgombea lipo suala la kupata na kukosa kuchaguliwa jambo la muhimu kwa sasa ni wajumbe kushikamana ili kuleta maendeleo mazuri ndani ya chama na siyo marumbano.
"Tuondoe chuki, baada ya uchaguzi kinachotakiwa katika chama ni mshikamano wenye kutenda,utekelezaji na kupata mafanikio mazuri yatakayoleta maendeleo" amesema Kainamula
Naye katibu wa UWT mkoa wa Kagera Rehema Zuberi amesema awali watia nia wa nafasi wa viti Maalumu walijitokeza wakiwa 13 mmoja kati ya hao hakurudilisha fomu.