Serikali yasimamisha huduma za upachikaji figo katika hospitali za Mediheal

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Afya Nchini Kenya Aden Duale, amesimamisha huduma zote za  upachikaji figo katika hospitali za Mediheal kufuatia madai ya ukiukaji sheria.

Akizungumza leo Alhamisi katika jumba la Afya Jijini Nairobi, Duale amesema kuwa agizo hilo limesababishwa na malalamishi kuhusu taratibu za upachikaji figo katika hospitali ya Mediheal tawi la Eldoret.



Duale alisisitiza kujitolea kwa wizara ya afya kulinda usalama wa wagonjwa  na kurejesha imani ya umma katika huduma za matibabu nchini Kenya.


Wakati huo huo,waziri Duale ameunda kamati huru ya wataalam itakayofanya uchunguzi kamili kuhusu huduma za upachikaji figo katika hospitali zote za  Mediheal zilizotolewa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuwasilisha ripoti yake katika muda wa siku 90 zijazo.


Kamati hiyo ina Jukumu la kuchunguza mifumo ya usimamizi ya hospitali hizo, utendakazi wa kliniki, kubainisha iwapo zimetimiza mahitaji ya kimaadili na taratibu za kiusalama za wagonjwa.


Waziri huyo amemsimamisha kazi Dkt. Maurice Wakwabubi ambaye ni kaimu mkuu wa kitengo cha utoaji na uhifadhi wa damu na huduma za upachikaji viungo Nchini Kenya na Dkt. Everlyne Chege, mwenyekiti wa kamati ya kiufundi ya wizara ya afya iliyofanya uchunguzi wa kinidhamu kuhusu swala hilo mwezi Disemba mwaka  2023.



Dr. Martin Sirengo, Naibu Mkuu Mkurugenzi wa huduma za matibabu sasa ndiye kaimu mkuu wa kitengo cha utoaji uhifadhi wa damu na upachikaji wa viungo vya mwili katika Wizara ya afya. 


Katika mkutano huo, Duale alikuwa ameandamana na katibu wa idara ya afya ya umma Mary Muthoni, Mwenzake wa huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga na Mkurugenzi wa Afya Dkt. Patrick Amoth. 




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top