Jwtz Brigedi ya Faru Yafanya Makubwa Zoezi la Medani Pima Uwezo 2025

GEORGE MARATO TV
0


 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Brigedi ya Faru  limehitimisha zoezi la medani PIMA UWEZO 2025 lillofanyika   Mkoani Shinyanga.

Akimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda katika kilele cha kuhitimisha zoezi hilo,Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu Meja Jenerali Fadhili Omary Nondo amewataka Maafisa na Askari kuwa tayari nyakati zote kulinda mipaka ya aridhini,angani na kwenye maji dhidi ya uvamizi wa adui.  

" Mazoezi ni sehemu ya kutufanya Wanajeshi tuwe tayari nyakati zote katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa Taifa ,hivyo wakati wa amani tunapaswa kuvuja jasho jingi ili wakati wa Vita tutekeleze majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa"

Aidha amesema  mazoezi haya yataendelea kufanyika kwa nyakati na sehemu tofauti nchini  kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa na Askari wa JWTZ.

Kwa upande wake Kamanda wa Brigedi ya Faru Brigedia Jenerali Gabriel Elias Kwiligwa  amesema zoezi hili limefanyika kwa siku 12 likiwa na lengo la kupima utayari wa vikundi katika kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, uvamizi wa vikundi kutoka ndani na nje ya nchi na kuzuia uhamiaji haramu.

Zoezi la Medani PIMA UWEZO 2025 lenye kauli mbiu isemayo"  PIMA  UWEZO,KAA TAYARI TUILINDE TANZANIA"  lililofanyika Mkoani Shinyanga pia  limeshirikisha   Askari wa Jeshi la Akiba(Mgambo).




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top