Jinsi Waziri Mkuu Majaliwa "Alivyoamisha" Ajenda ya No Reforms No Election ya Chadema Jijini Mbeya Jana!

GEORGE MARATO TV
0


 

George Michael Uledi!

Ni mambo mawili tu ambayo yalitawala katika ufunguzi wa Mikutano ya Chadema(NO REFORMS NO ELECTION)ambayo RASMI ilizinduliwa JIjini Mbeya Jana na Timu ya viongozi waandamizi wote wa Chadema Taifa!

Ni kama vile ajenda ya No Reforms No Election imezikwa RASMI na MAONO ya Mh Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kuhusu umuhimu wa Vijana kwenda kupata Elimu ya ujuzi kutoka  VETA baada ya Chadema Jana kutumia muda mwingi kutaka kuisambaratisha hoja ya Mh Waziri Mkuu Majaliwa bila mafanikio!

Tafiti zinaonyesha(Labour Force Estimates Survey 2025,NBS) kuwa kati ya wahitimu wa VETA (10), wahitimu saba mpaka wanane(7-8) either wamejiari,wameajirika hivyo kuikana taarifa ya Chadema ya Jana Mkoani Mbeya kwamba wahitimu wa VETA bado hawaajiriki!No Research No Right to Speak!

Kuonyesha kwamba Kauli yao ya No Reforms No Election "imedunda" Mkoani Mbeya Jana,kati ya watu (10) waliohojiwa kuhusu ufahamu wa MSIMAMO huo wa Chadema(No Reforms No Election),ni mtu mmoja(1) tu ambaye alionyesha kwanza uelewa wa kauli hiyo na pili KUKUBALIANA na kauli hiyo!Karibia watu (9) kati ya watu (10) waliohojiwa baada ya Mkutano huo kuisha walionyesha kutokuamini kuwa Chadema wanaweza kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025!


KAULI YA WAZIRI MKUU MAJALIWA BADO "INASIMAMA"

Karibia asilimia 98% ya mafundi wa Magari kwenye magereji yetu pale mfano eneo la Soweto JIjini Mbeya wanaishi kwa kutumia "ujuzi" wao either kwa kusoma VETA au kwa kujifunza kazini!

Kama mfano ukafanya utafiti leo wa "Labor Force Employability in Tanzania",kwa kuangalia "Assessing factors Accelerating Employment in Tanzania" ni wazi kuwa "ujuzi" ndio utakuwa sababu kubwa wa watu wasio na Elimu kubwa kuweza kuajirika!

Lakini pia ni wazi kuwa "UJUZI-SKILLS" unaajiri mara (10) zaidi ya "TAALUMA"!Ukweli unabaki kuwa ukweli!

Nitoe changamoto hapa kwa National Bereau of Statistics (NBS) kufanya utafiti haraka wa "UJUZI vs TAALUMA" kwa kuangalia kipi kinaajiri watu wengi(Vijana) zaidi kwa sasa na uelekeo wa soko la ajira Nchini Tanzania miaka (20) ijayo!

Asante Mh Waziri Mkuu kwa kuibua mjadala mzito ndani ya Nchi yetu ya Tanzania ambao sasa umewafanya hata Chadema kusahau kabisa jana malengo makuu ya ajenda yao ya No Reforms No Election!

"Ukubwa" wa mtu upimwa kwa MAONO MAONI na MAWAZO yake!PM Majaliwa ameonyeaha "misuri yake" ya kifalsafa!

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa apewe "PhD yake" haraka sana!Vyuo Vikuu mpo?🤷🏻‍♂️🤷🏻‍♂️


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top