Nitakuwa Mkali Sana Kwa Wala Rushwa na Wanaotumia Vibaya Madaraka yao-Rc Tabora

GEORGE MARATO TV
0


Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Paul Chacha amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa huduma ya ununuzi serikalini(GPSA) wa Mkoa huo Mayala Ambuli pamoja na Watumishi Wawili wa Wakala wa Barabara(Tanroads)kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili. 

Chacha amechukua hatua hiyo baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa Wateja wa GPSA Mkoani Tabora  pamoja na viongozi akiwemo yeye binafsi kuwa Muhanga wa Lugha ambazo hazina staha kutoka Ndugu Mayala.

"Leo asubuhi nimefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya Wakala wa huduma ya ununuzi Serikalini (GPSA)- Mkoa wa Tabora, nikiwa Katika ziara hiyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora nimemsimamisha Kazi kupisha Uchunguzi Ndugu Mayala Ambuli ambaye alikuwa ni Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora kwa tuhuma za Kutumia Madaraka yake vibaya, Kutoa Lugha Zisizo na Staha kwa Wateja wa GPSA na Viongozi wa Serikali na kuwa na Utovu wa nidhamu Kazini"Alisema Chacha Wakati wa kikao hicho. 

Pia, Mkuu wa Mkoa Tabora Paul Chacha amefanya ziara ya Kushtukiza katika Ofisi ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kufanya kikao kifupi na Watumishi wa Ofisi hiyo ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Mhandisi Rafael kuwatoa watumishi wawili wa Mzani mdogo wa Tuli ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za kupokea rushwa zinazowakabili.

Chacha amewaasa watumishi wote wa Mkoa wa Tabora, kufanya kazi kwa kufuata Taratibu na misingi ya utumishi wa Umma. 

"Nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora sitakubali mtu yeyote yule kufanya makosa hasa ya Matumizi mabaya ya madaraka kwa manufaa yao binafsi, nitakuwa Mkali muda wote kwa watumishi wa aina hiyo" Alionya Chacha

Aidha amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Tabora kwa kuendelea kumpa Ushirikiano ikiwemo kumpatia taarifa moja kwa moja juu ya watumishi ambao wanatumia vibaya ofisi zao au maeneo yao ya kazi na kuwahakikishia Wananchi kuwa watumishi wote wameletwa Tabora kwa ajili ya kuuwatumikia na sio kutumikia madaraka yelao ikiwemo  kuwaonea Wananchi wa Mkoa huo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top