Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Ndugu Kassim Majaliwa leo Februari 15, 2025 ni mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu Maalum Chama cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu.
Mkutano huo maalum mbali na kuhudhuriwa maelfu ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa jimbo la Itilima lakini pia umehudhuriwa na mamia ya wana CCM,wapenzi na wakeleketwa wa chama hicho wakiwemo viongozi mbalimbali wa chama, Serikali na viongozi wa dini.