Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Bukoba wapewe Onyo Kali

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian; Bukoba

WENYEVITI na wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kutowatoza wananchi kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia huduma pale wanapofika katika ofisi za Serikali ya mitaa na kata bali fedha hiyo iwe inatambulika kisheria.

Wito huo umetolewa na  Meya wa Manispaa hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Nshambya Godsoni Gibsoni wakati akiongea katika mafunzo aliyoyaanda yeye ya kuwajengea uwezo na kuwapa vitendea kazi  viongozi wa mitaa katika kukuza maendeleo ya wananchi na kuwapongeza kwa kuchaguliwa.

Gibson amesema baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatozwa ela kiasi cha shilingi 5,000 wanapokwenda kupata huduma kwa wenyeviti,wajumbe na watendaji kwa ajili ya kupata huduma hivyo ndipo akaamua kutoa vitendea kazi ikiwemo karatasi kwasababu wapo wananchi ambao hawana ela hiyo. 

"Inawezekana inatolewa hiyo ela wasababu ya ulipaji wa ada kwa ajili ya kununua karatasi,uchapaji wa barua,kwenda kuangalia tukio kunahitajika gharama hivyo mimi kama diwani wa Kata Nshabya nimeamua kufadhili ofisi zetu za mitaa mitatu  kutoa vifaa ambavyo ni karatasi limu tisa,stamp pad kwa ajili ya kugonga mhuri,karamu na mahitaji mengine na hili litakuwa endelevu pale wanapoishiwa wanijulishe niwapatie vifaa hivyo"ameeleza Gibson


Anasema nia yake ni kuhakikisha mwananchi yoyote wa kata ya Nshambya asitozwe hata shilingi moja ili kupata huduma inawezeka wengine wakachukia lakini, nia hii ni kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kama inavyostahili.

Amesema viongozi hao wamejifunza mada sita zinazohusu wajumbe na wenyeviti wa Serikali za mitaaa ili watambue majukumu yao ambazo zimetolewa baada ya kumaliza uchaguzi wa Serikali za mitaa lengo kubwa waweze kupeleka huduma bora kwa wananchi na kutambua majukumu yao.          

 Naye Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Proscovia Mwambi akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amewataka viongozo hao  kuyafanyie kazi mafunzo hayo kwakua wazalendo na waadilifu katika kuwahudumia wananchi na kutotumika tofauti na malengo ya Serikali kwani wao ni kiungo muhimu kwa wananchi na Serikali.

Mjumbe wa mtaa Bunkango kata Nshabya  Anna Mshumbuzi  akaiongea kwa niaba ya viongozi wa mtaa ambao wamepatiwa mafunzo na vitendea kazi akaeleza kwa namna gani maafunzo hayo yatakavyo enda  kuwasaidia katika utendaji kazi wao ambapo amesema  wametakiwa kuwafichua  wazazi ambao mpaka sasa hawajawapeleka watoto shule ili wachukuliwa hatua 

Semina hiyo ambayo imefanyika katika chuo cha King Rumanyika Manispaa ya Bukoba imejumuisha wenyeviti wa serikali za mitaa,wajumbe na watumishi kutoka kata ya Nshabya mkoani humo.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top