Uwanja wa Ndege Musoma Kuendelea na Ujenzi Wake Wiki Ijayo

GEORGE MARATO TV
0


 

Na Shomari Binda-Musoma

UJENZI wa upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma unatarajiwa kuendelea wiki ijayo baada ya taratibu mbalimbali kukamilika.

Hii imekuwa habari njema kwa wawekezajj wa biashara ya utalii wakiwemo wa hotel na watumiaji wengine wa uwanja huo.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii meneja wa TANROADS mkoa wa Mara mhandisi Vedastus Maribe amesema ujenzi huo utaendele na matarajio ni kwenda kwa kasi.

Amesema yapo mambo ambayo yamekamilishwa na serikali ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia kwa wananchi na kutoa nafasi ya kuendelea na ujenzi huo.

Mhandisi Maribe ameishukuru serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na zikiwemo za fidia kwa wananchi ambao tayari wameanza kulipwa.

Amesema wao kama wasimamizi watasimamia na kufatilia kwa weledi mkubwa ili kuona uwanja huo unakamilika.

" Tutaendelea na ujenzi wiki ijayo na tunatoa shukrani kwa serikali yetu chini ya Dkt.Samia kuhakikisha tunaukamilisha ujenzi huo",amesema.

Katika siku za hivi karibuni wawekezaji wa sekta ya utalii waliiomba serikali kuuangalia uwanja huo ili uweze kukamilishwa na kutoa fursa za kufanyika vyema kwa shughuli za utalii.

Mkurugenzi wa Le Grand Victoria Hotel ya mjini Musoma Ramadhan Msomi Bwana amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa usikivu na na kujibu kwa wakati na sasa ujenzi unakwenda kuendelea.

Wakati wa kukabidhiwa hundi ya fedha kwa wananchi wanaopisha ujenzi huo wa maeneo ya Nyasho na Kamnyonge mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo alitoa wito kwa wananchi wanaopata fedha hizo kutumia kwa malengo mazuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha makazi mapya.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top