Waziri Kombo akutana na Balozi wa Korea nchini

GEORGE MARATO TV
0

 

🇹🇿🇰🇷Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Ahn Eun-ju, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.


Viongozi hao walijadili kuhusu namna bora ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea ambao umedumu kwa takriban miaka 32 sasa.


Ikumbukwe kuwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Korea iliyofanyika tarehe 31Mei hadi 6 Juni , 2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Yoon Suk-Yeol, Rais wa Jamhuri ya Korea walishuhudia utiaji saini wa Hati nne za Makubaliano zilizolenga kukuza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uchumi wa buluu, Madini ya Kimkakati na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania kupitia Mkataba wa Masharti nafuu wa Dola za Marekani bilion 2.5 kwa kipindi cha mwaka 2024-2028.



Viongozi hao walisisitizia umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea ili kufanikisha utekelezaji wa makubaliano hayo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top