Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, ameongoza Maafisa, Askari na Waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, enzi za uhai wake alishika nafasi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kuanzia mwaka 2018 hadi 2019.
Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, alifariki dunia tarehe 24 Desemba 2024, katika hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili Dar es Salaam na kuagwa leo tarehe 27 Desemba 2024 na kusafarishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Nyegezi, Mwanza tarehe 28 Desemba 2024.