Zaidi ya madereva 90 wafungiwa leseni

GEORGE MARATO TV
0


 Na Dawati la Habari Polisi Mwanza

Jeshi la Polisi nchini limewafungia leseni za udereva madereva 95 kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo kuendesha magari yao kwa mwendokasi.

Hayo yamebainishwa Oktoba 22, 2024 na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhan Ng'anzi alipofanya ziara ya kikazi Jijini Mwanza.

Akizungumza na madereva, abiria na wananchi katika Kituo Kikuu cha Mabasi Nyegezi na Nyamhongoro mkoani humo DCP Ng'anzi amesema ziara hiyo imelenga kutoa elimu kwa madereva na makundi mengine ya watumiaji wa barabara ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

Aidha, DCP Ng'azi amesema, atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria madereva wote ambao hawatazingatia sheria za usalama barabarani hususan  kwa madereva wanaoendesha gari kwa mwendo kasi na makosa mengine hatarishi.



Huku akitaja magari yaliyokamatwa DCP Ng’anzi amesema; “Magari yaliyokamatwa kwa kukosa taa ni 2,250, magari 4,405 wamekamatwa kwa kuzidisha abiria, magari 30 wamekamatwa kwa abiria kushindwa kufunga mikanda, mgari 12,000 yamekamatwa kwa ubovu"

"Tumewakamata madereva walevi zaidi ya 40,  tumekamata magari zaidi ya 5,000 kwa kosa la mwendo Kasi pamoja na pikipiki zaidi ya 3,000 ambazo dereva na abiria wake hawakuvaa kofia ngumu" amesema DCP Ng'anzi 

Kwa upande wake mwenyekiti wa usalama barabarani Fredinand Chacha amesema; “Imekuwa desturi kwa  madereva wengi wanapoendesha vyombo vya moto kutumia vilevi na kuchochea ongezeko la ajali kutokea barabarani.

"Matatizo mengi ni madereva wengi wanakuwa wameshakunywa madawa yao wengine wamesizia wengine huendesha rafu lakini kwa sababu upo mkakati wa kuwa dhibiti madereva wa tabia hizo nakuhakikishia ajali zitapungua" amesema Chacha.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top