WAUMINI WAMZAWADIA KATEKISTER PIKIPIKI

GEORGE MARATO TV
0


Waumini wa Kigango Cha Mt. Petro Masawe Parokia ya Misungwi wakishikiana na Wafadhili wamemzawadia Katekister Elias Kabipe Zawadi ya Pikpikipi katika Sherehe ya Somo wa Makatekster Mt.Yakobo Mwaka 2024 iliyofanyika Tarehe 31/8/2024 Kigango cha Mt.Petro Masawe Parokia ya Misungwi iliyotanguliwa na adhimisho la Misa Takatifu.

Akizungumza katika Sherehe hizo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Kigango Cha Mt.Petro Masawe Be.Thomas Lutego ameeleza kwamba Waumini hao kwa kushirikiana na Wadau na Wafadhili wameamua kumpatia Pikipiki Aina ya San LG 125 yenye thamani ya shilingi 2,350,000/= ili kumsaidia kutoa huduma ya Utume kwa Waumini kwa urahisi zaidi kwenye Jumuiya ndogo ndogo saba za Kigango hicho zenye Waumini zaidi ya 300.


Kwa upande wake Paroko Msaidizi wa Parokia ya Misungwi Padri William Leba amewapongeza Waumini hao na kuwasihi kuendeleza Umoja na ushirikiano ili kuendeleza kumtukuza Mungu na kuongeza juhudi ya Kazi na uwajibikaji katika Kanisa Katoliki.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top