Wahitimu darasa la saba waonywa kupokea zawadi zinazoweza kukatisha ndoto zao

GEORGE MARATO TV
0


Mwandishi wetu Mwanza

Mjumbe wa Bodi ya Shirika la EMEDO Bwana Edwin Soko amewataka wahitimu wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Sweya kujiepusha na vishawishi vya zawadi na fedha toka mitaani wakati huu wanaposubiri matokeo yao ya kuendelea na masomo ya Sekondari.

Soko ameyasema hayo alipokuwa Mgeni rasmi kwenye maafali ya 21 ya Shule ya Msingi Sweya, iliyopo kata ya Luchelele, Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Soko alisema kuwa, Kwa sasa kuna vishawishi vingi huko  Mitaani na wajibu wao wahitimu kujilinda na vishawishi hivyo ili waendelee kubaki salama na kuendelea na masomo yajayo ya Sekondari.

Soko pia aliwataka wazazi kuwalinda watoto wawepo Nyumbani maana vitemdo vya ubakaji na ulawiti vinazidi kuongezeka na watoto ni kundi lililo kwenye hatari.

Edwin Soko alikuwa Mgeni rasmi aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Shirika la EMEDO alisema shirika hilo litatoa mashine ya kurudufusha karatasi (Photocopy machine ) ili kutatua changamoto za kitaaluma shuleni hapo.

Jumla ya wahitimu 102 walipewa vyetu vya kuhitimu darasa la Saba na vya umahiri wa masomo mbalimbali.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top