SERIKALI KUJENGA SKIMU YA UMWAGILIAJI WILAYANI IRAMBA

GEORGE MARATO TV
0


 Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) imewaelekeza wataalam wake kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kupata mahali pa kujenga skimu ya Umwagiliaji katika bonde la Ulemo-Nzinziligi-Mbelekese lililopo wilayani Iramba Mkoani Singida.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Raymond Mndolwa ametoa maelekezo hayo wilayani Iramba wakati akimuonesha Waziri wa Fedha Dokta.Mwigulu Nchemba ramani ya Jiografia ya Bonde hilo.


Kwa mujibu wa Mndolwa,Baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu,Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika bonde hilo utakaohusisha Bwawa,uchimbaji wa visima pamoja na Miundombinu ya umwagiliaji.


Bonde la Ulemo-Nzinziligi-Mbelekese lina ukubwa wa hekta 43,000 ambapo Ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji unatarajia kunufaisha wakulima katika kata sita za Ulemo,Ndago,Mbelekese,Mukulu,Kaselya pamoja na Kiengege.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top