Mhandisi Kundo Methew Awataka Wananchi Bukoba Kulinda na Kutunza Miundombinu ya Miradi ya Maji

GEORGE MARATO TV
0

 


Na Angela Sebastian-Bukoba 

Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amewataka wananchi katika wilaya ya Bukoba kunakochimbwa visima jumla ya 15 kulinda na kutunza miundo mbinu inayojengwa katika maeneo kunakochimbwa visima hivyo.

Amesema hiyo itasaidia  kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu na inatoa huduma ya maji kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.

Mhandisi Methew amesema hayo baada ya kushuhudia uchimbaji wa kisima cha maji katika kata ya Kyaitoke   wilaya ya Bukoba ambapo pia aliizungumza na wananchi wa kata hiyo, akawaasa wananchi kunakochimbwa visima 15 kulinda miundombinu ya maji itakayojengwa katika maeneo yao.

 Evodius Ishengoma ni mwananchi wa kata hiyo aliishukuru serikali kwa kuona umuwa kuchmbq kisima hicho katika maeneo yao ambapo itasaidia kuepuka adha ambayo wanaipata  ya kutumia maji ya madimbwi ambayo si salama kwa Afya zao maana visima vilivyokuwepo awali vimeharibika.

Uchimbaji wa kisima  kimoja unagharimu kati ya shilingi milioni 30 hadi 41 ambapo mpaka sasa na visima 10 tiyali vinechimbwa huku vitano vikiendelea kukamilishwa.

Ko


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top