Na Shomari Binda-Musoma
JESHI la Polisi Wilaya ya Musoma limetambua mchango uliotolewa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kufanikisha mashindano ya Polisi Jamii Cup 2024.
Kabla ya kuanza mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 20 mbunge huyo alitoa ng'ombe kama zawadi kwa bingwa na mipira 16.
Cheti cha pongezi cha kutambua mchango huo kimetolewa jana septemba 29 na mgeni rasmi wa fainali ya mashindano hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi Nenrad Sindano
Amesema wanatambua mchango wa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo na moyo wake wa upendo na kujitoa katika masuala ya kijamii.
Sindano amesema lengo la mashindano hayo limefanikiwa kwa kuwa elimu juu ya utoaji wa taarifa juu ya uhalifu na wahalifu ikiwemo ushiriki wa uchaguzi wa serikali za mitaa ilitolewa.
Amesema vijana na wote waliopsta elimu kupitia mashindano hayo wanapaswa kuishi nayo na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
" Mashindano yetu yamemalizika salama ujumbe umetolewa na umewafikia wananchi twende tukashirikiane kuhakikisha tunakomesha vitendo vya uhalifu.
" Huu ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa tukashiriki kwa amani bila kujiingiza kwenye matukio ya kuvuruga uchaguzi",amesema.
Akizungumza na GMTV mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameshukuru jeshi la polisi Wilaya ya Musoma kwa kutambua mchango wake
Amesema kama kiongozi anapaswa kushirikiana katika masuala ya kijamii na kuendelea kutoa ushirikiano popote atakapo hitajika.
Licha ya mbunge Mathayo wadau mbalimbali wamekabidhiwa vyeti vya pongezi na jeshi la polisi Wilaya ya Musoma kwa kutambua mchango wao.
Katika fainali hiyo timu ya Mars Sport Academy wameibuka mabingwa kwa kuifunga timu ya Mshikamano bao 1-0