Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimemtunuku Nishani ya miaka 60, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda.
Mbali na mkuu huyo wa najeshi,wengine waliotunukiwa ni Majenerali, Maafisa pamoja na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi.
![]() |