TRC Kujitegemea: Serikali Kufuta Ruzuku ya Mishahara 2026/27

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI wa Uchukuzi, Makame Mbarawa, amesema Serikali haitaendelea kutoa ruzuku ya mishahara kwa Shirika la Reli Tanzania (Tanzania Railways Corporation (TRC)) kuanzia mwaka wa fedha 2026/2027, kufuatia mafanikio ya maboresho makubwa yaliyofanyika ndani ya shirika hilo tangu kuanza kwa mageuzi yake mwaka 2017.

Akizungumza leo Mei 13, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Prof. Mbarawa amesema hatua hiyo ni ishara ya kuimarika kwa ufanisi na uwezo wa TRC katika kujitegemea kiutendaji na kifedha.





Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa uliowekwa katika kuliboresha shirika hilo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha sekta ya reli nchini kwa lengo la kuongeza ufanisi wa usafiri na kuchochea maendeleo ya uchumi.

“Tangu kuanzishwa kwa shirika hili, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya mishahara. Hivyo naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 TRC haitatengewa tena ruzuku ya mishahara kutoka Serikalini,” amesema Prof. Mbarawa.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya mageuzi ya muda mrefu yanayolenga kulifanya shirika hilo liendeshe shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kupunguza utegemezi wa fedha za Serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top