Dkt Mwigulu Afungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Ziwa Tanganyika

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 16, 2026 amefungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Ziwa Tanganyika (The Lake Tanganyika Business and Investment Forum) linalofanyika mkoani Kigoma.

Kongamano hilo linalowakutanisha viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika, zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, ni miongoni mwa mikakati ya kuuwezesha mkoa wa Kigoma na ukanda huo kuwa kitovu cha biashara itayosaidia kupiga hatua zaidi za maendeleo endelevu.

Akizungumza katika Kongamano hilo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa kongamano hilo litaibua matumaini mapya ya ushirikiano wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.









Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa mkoa wa Kigoma una fursa na rasilimali nyingi ambazo bado hazijatumika ikiwemo ardhi kubwa yenye rutuba, vivutio vya utalii, madini na viwanda vinavyotoa nafasi ya kuchochea uwekezaji mkoani mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top