DODOMA.
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Maji Bonde la ziwa Victoria Dkt. Renatus James Shinhu, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda vyanzo vya maji, kutunza miundombinu iliyojengwa, kuzuia uchafuzi wa mazingira na kutumia rasilimali za maji kwa uangalifu kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Amesa ulinzi wa rasilimali za maji haupaswi kuwa jukumu la taasisi za serikali pekee, bali unahitaji ushiriki wa wananchi wote katika kuhifadhi mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dodoma wakatika akieleza Mafanikio yaliyopatikana katika siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dk. Renatus Shinhu ameeleza kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua kuwa maji ni maisha na ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya jamii, hivyo kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ni jukumu la kila mmoja ili kuhakikisha rasilimali hiyo inaendelea kuwepo kwa matumizi endelevu.
"Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria itaendelea kusimamia rasilimali hizi muhimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, kwa kufuata maelekezo ya Serikali na kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo". Amesema
Aidha, Dk. Renatus amesema kuwa Bodi kupitia mradi wa ujenzi wa mabwawa, imejenga mabwawa mawili likiwemo la Bugarama lililopo Kata ya Iyogelo na bwawa la Mwamashindike lililopo Kata ya Mwabaraturu wilayani Maswa ambayo yanatumika kwa matumizi ya binadamu, mifugo na kilimo cha umwagiliaji.
"Bodi kupitia mradi wa usimikaji wa Vituo vya Ufuatiliaji wa Maji, imesimika vituo vya kufuatilia mwenendo wa maji katika mito ya Duma, Mori, Ngono, Mwisa na Kagera (Nyakanyasi), mabwawa ya New Sola na Manchira pamoja na kituo kimoja katika Ziwa Victoria". Amesema
"Vituo hivyo vinakusanya takwimu za mtiririko, ujazo na kina cha maji ili kusaidia maamuzi ya kitaalamu kuhusu mafuriko, ukame na upangaji wa matumizi ya maji". Amesisitiza
"Miradi inayotekelezwa na Bodi imenufaisha wananchi, taasisi za umma, wakulima, wafugaji na wadau wa maendeleo kwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama mijini na vijijini, kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na shughuli za ufugaji, kupatikana kwa takwimu sahihi za kitaalamu kwa ajili ya maamuzi ya kisera na kiutendaji pamoja na kupunguza migogoro ya matumizi ya maji.". Ameongeza
Sambamba na Hayo,.amesema Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria itaendelea kusimamia rasilimali hizi muhimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, kwa kufuata maelekezo ya Serikali na kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo.
Bodi ya Maji Bonde la ziwa Victoria ina jukumu la kusimamia, kulinda na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za maji ndani ya Bonde la Ziwa Victoria ambapo moja ya majukumu yake ni kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji kupitia ukaguzi na ufuatiliaji wa matumizi ya maji katika mito, mabwawa na vyanzo vingine.




