Uzalishaji na Usambazaji Bidhaa Bandia Kunahujumu Mapato ya Serikali na Kudhorotesha Maendeleo Nchini

GEORGE MARATO TV
0


Na mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma.

Uzalishaji na usambazaji bidhaa bandia kuna hujumu mapato ya Serikali na kudhorotesha Maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa na afisa ukaguzi bidhaa bandia kutoka tume ya ushindani(FCC) Mgasi  Kalindimya wakati akitoa elimu kwa wananchi na wanafunzi waliofika katika banda lao viwanja vya shule ya msingi Mukendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Katika wiki ya haki ya mlaji FCC wapo katika viwanja hivyo kuanzia Machi 19-27, 2026 ambapo maafisa kutoka katika tume ya ushindani wanatoa elimu kwa wananchi.

Mgasi amesema kuwa kumekuwa na utitiri wa bidhaa bandia kwa wauzaji ambao wengi wanasambaziwa na wafanyabiashara wasio waaminifu ambao hawafuati taratibu za kisheria ikiwemo Sheria ya alama ya bidhaa na kanuni zake.

Akifafanua sheria hiyo amesema bidhaa bandia nyingi zina madhara kwa watumiaji na uchumi wa nchi ambapo Serikali imekuwa ikipoteza mapato(Kodi) na kudhorotesha Maendeleo.

"Vilevile bidhaa hizo zinz madhara kwa mlaji ambapo inapelekea kuathiri afya ya mlaji na kusababisha maradhi yanayoweza kuondoa uhai wa mlaji pia kwa bidhaa za vyombo vya moto vinapelekea ajali mbalimbali,amesema Mgasi.

Kwa Upande wake afisa mkaguzi wa bidhaa bandia Thomas Maisory   amesema kuwa uzalishaji na usambazaji bidhaa bandia ni kosa kisheria kwa mujibu wa sheria kifungu cha 9 cha Sheria ya alama ya bidhaa cha Mwaka 1963 kama ilivyofanyiwa marekebisho.

Amesema Wauzaji na wasambazaji wakikamatwa hutozwa faini au kufikishwa mahakamani kulingana na thamani ya mizigo  iliyokamatwa.

Utoaji wa adhabu hiyo hufuata muongozo na kanuni zilizopo ikiwemo uteketezaji bidhaa hizo ndani ya mwezi mmoja  lengo ni kuthibitisha na kujilizisha na uhalali wa bidhaa hiyo.

Thomas ametoa wito kwa wananchi kufika katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo ili wapate uelewa mpana wa bidhaa bandia kuepuka madhara ya kiafya hapo baadae na kuokoa hasara kwa Wauzaji.

Baadhi ya wananchi waliofika katika viwanja hivyo Lima, Dominic, Charles Masuna na Magari Hassan wameiomba tume kuweka utaratibu wa elimu endelevu ili kuwasaidia walaji na kuwaepusha na madhara na hasara lakini pia wamesema watakwenda kuwa mabalozi kwa wengine wafike kupata elimu kwa usahihi zaidi.

Aidha Charles  Masuna amesema kuna haja ya  wananchi kuwa na mwamko wa kuchangamkia fursa za elimu kwa maslahi yao.

Kauli mbiu ya Mwaka huu inasema kuwa Bidhaa Salama, Imani kwa mlaji".


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top