Benki ya Azania imezindua rasmi mashine ya kutolea fedha kiotomatiki (ATM) katika eneo la Arusha International Conference Centre (AICC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki wa kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Bi. Christine Mwakatobe, Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC alisema kuwa uwepo wa ATM hiyo AICC utatatua kwa kasi kubwa changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha iliyokuwa ikiwakabili wadau na wageni wa kituo hicho.
Naye Bw. Yahaya Mbanka, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania, alisema kuwa ushirikiano kati ya Benki ya Azania na AICC unalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wageni, washiriki wa mikutano pamoja na wafanyabiashara wanaotembelea kituo hicho maarufu cha mikutano.
@azaniabankplc
#benkiinayozidimatarajio









