Agnes Marwa Awakumbuka Wafungwa Gereza la Musoma Mjini

GEORGE MARATO TV
0


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, ametembelea Gereza la Musoma Mjini na kutoa misaada mbalimbali kwa wafungwa wa dini ya Kiislamu na Kikristo ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.

Katika ziara hiyo, Mbunge Marwa alikabidhi mahitaji muhimu yakiwemo tambi, sukari, tende, sabuni pamoja na mitandio maalum kwa wafungwa wa kike, msaada uliolenga kuboresha ustawi wao wakati wa kipindi cha ibada.

Aidha, alipata fursa ya kuzungumza na kusikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa wafungwa, ambapo walimweleza hitaji lao la kupatiwa king’amuzi kitakachowawezesha kufuatilia vipindi na matukio mbalimbali kupitia televisheni. Akijibu ombi hilo, Agnes Marwa alikubali kulitekeleza na kulipia hapo hapo king’amuzi kwa miezi yote iliyosalia ya mwaka huu, hatua iliyopokelewa kwa furaha na shukrani kubwa kutoka kwa wafungwa.

Katika ziara hiyo,Agnes Marwa aliambatana na Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Mara chini ya uongozi wa Katibu wa UWT Mkoa, Ndeni Amos,Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Ndg Noela Gachuma pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Musoma.


Akizungumza na wafungwa na uongozi wa Gereza, Agnes Marwa alisisitiza kuwa Ramadhani na Kwaresma ni nyakati za kujitafakari, toba na kusaidiana, hivyo jamii ina wajibu wa kuwajali wote bila ubaguzi.

“Tumekuja kuwafariji na kushiriki nanyi katika kipindi hiki cha ibada. Tunatambua mahitaji yenu na tutaendelea kushirikiana nanyi ili kuwapa faraja na matumaini,” alisema Marwa.

Uongozi wa gereza pamoja na wafungwa walitoa shukrani zao kwa msaada huo, wakieleza kuwa umeongeza faraja, motisha na hisia za kuthaminiwa na jamii. Hatua hiyo inaendelea kuonesha dhamira ya Mbunge Agnes Marwa ya kuwagusa makundi mbalimbali ya jamii na kuimarisha mshikamano katika Mkoa wa Mara.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top