Tanapa Kutumia Zoezi la Urushwaji Wa “Fash Fash” Kunadi Vivutio Vyake

GEORGE MARATO TV
0


Na. Jacob Kasiri - Zanzibar.

TANAPA kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na  Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) watia nanga eneo la Forodhani leo Januari 11, 2026 kwa lengo la kunadi vivutio vya utalii pamoja na fursa za uwekezaji.

Eneo la Forodhani ni maarufu sana Zanzibar kwa kuwa na wageni kedekede kutoka mataifa mbalimbali kuja kushuhudia shughuli za utalii zinazotekelezwa katika eneo hilo, pia eneo hilo limepokea meli kubwa ya kitalii ya M/S Azamara (Cruise ship) iliyotokea Mauritania ikiwa na watalii 668 na crews 368.

Hivyo uwepo wa TANAPA, TTB sanjari na Kamisheni ya Utalii Zanzibar kama mwenyeji wa eneo hilo ni fursa adhimu na mjarabu ya kunadi vivutio vya utalii kama vile utalii wa wanyamapori na fursa za utalii.

TANAPA wapo Kisiwani Unguja katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Dimani - Fumba, Zanzibar, aidha pia shirika hilo linatarajia kushiriki shamra shamra za Sikukuu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo usiku kwa kushuhudi  urushwaji wa “FASH FASH” itakapotimu saa 6:00 usiku wa leo Januari 11, 2026.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top