Maafisa Habari Wasioendana na Kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita "Kitanzini"....

GEORGE MARATO TV
0

  

Serikali imewataka maafisa habari nchini kutumia teknolojia inayoendana na wakati na mazingira ili kuwafikishia wananchi habari sahihi kwa wakati.

Hayo amebainisha mapema hii leo, Disemba 17, 2025, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka katika ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili cha  kitaifa cha kurugenzi ya mawasiliano ya Rais na maafisa habari wa serikali  kilichoandaliwa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu ambapo  pia amewasihi maafisa hao kuepuka kutoa habari za kiongozi badala ya kutoa taarifa za serikali katika sekta husika jambo ambalo si Zuri kwa ujenzi wa taifa.

Aidha, Balozi Kusiluka amesema  kuwa ni muhimu kujipanga vizuri katika kukabiliana na matumizi hasi ya teknolojia ya habari katika kuleta maendeleo na ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.

Pia, Bolizi kusiluka amewataka maafisa habari nchini kutokuwa maripota wa matukio badala yake kuwa maafisa wa habari na mawasiliano na kuwa na maudhui yenye kujenga taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu, Bakari Machumu amesema kuwa serikali  ina maafisa habari zaidi ya 800 nchini hivyo hakuna sababu ya kukosa taarifa zenye mlengo wa kujenga jamii za kitanzania hivyo uwepo wa maafisa hawa ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya serikali katika kuwahudumia watanzania.

Naye, Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano kupitia , Tiddo Mhando amesema matarajio ya serikali ni kubadilishana mawazo katika kusaidia serikali katika kuboresha ubora wa taarifa katika sekta mbalimbali za serikali.

Pia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameishukuru serikali kwa kuina umuhimu wa kuwaunganisha maafisa habari jambo ambalo linalosaidia kuchochea utendaji kazi  wa maafisa habari katika sehemu zao za kazi.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top