Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ameielekeza VETA kujenga uzio katika Chuo cha VETA Chemba pamoja na kurejesha kozi za muda mfupi za kilimo na ufugaji zilizokuwa zimefutwa nchini ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya maeneo yao na kujiajiri baada ya kuhitimu.
Aidha, amesema serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kuiagiza taasisi hiyo kuzingatia ubora wa mafunzo ili yaendane na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mhe. Wanu ametoa maelekezo hayo Novemba 26, 2025, wakati wa ziara yake katika Chuo cha VETA Chemba pamoja na kuzindua ugawaji wa vifaa vya mafunzo kwa vyuo 63 vya VETA nchini. Kwa Kanda ya Kati, vyuo vya Chemba na Singida ndivyo vilivyopokea vifaa hivyo

















