Ndejembi Aja na Mikakati ya Kuisuka Kisawasawa Tanesco

GEORGE MARATO TV
0


 WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupanga mikakati ya kuboresha utoaji huduma kwa wateja, lakini pia kufanya tathmini ya utendaji kazi na kuweka mikakati mipya ya kuongeza kasi ya utoaji huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo Novemba 22, 2025 alipofanya kikao kazi cha pamoja na Watumishi wa TANESCO jijini Dodoma.

“ Ni maelekezo yangu kwa TANESCO kuhakikisha tunaboresha huduma zetu kwa watanzania lakini pia kuweka mikakati mipya itakayosaidia kuongeza kasi ya utoaji huduma pamoja na kuimarisha zaidi hali ya upatikanaji wa umeme.

Katika kikao hicho Mhe. Ndejembi ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu, Mhandisi Felchesmi Mramba pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top