TANZANIA inatarajia kuunganisha sekta binafsi za nchini na nchi ya Oman ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara hatua ambayo itawwzesha kukuza uchumi wa nchi na sekta binafsi kwa ujumla.
Hayo amebainisha Septemba 11, 2025, jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abassi Kilima katika ziara ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Oman katika Bandari kavu ya Kampuni ya PMM GROUP wenye lengo kutambua na kubadilidhana fursa mbalimbali za kibiashara baina Tanzania na Oman ambapo amesema lengo ni kushirikiana kibiashara kupitia PMM GROUP.
Aidha, Balozi Abdallah amesema matarajio ya serikali ni kuona ukuaji wa sekta ya biashara baina nchi hizi mbili baada ya kupatikana kwa usafiri wa uhakika baina ya Tanzania na Oman.
Katika hatua nyingine balozi Abdallah Abbasi Kilima amesema PMM group kwasasa ina takribani meli tatu hivyo uwepo wa meli hizo itakuwa ni kiungo muhimu katika kuunganisha biashara baina ya nchi hizo mbili.
Pia, Balozi Abdallah amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani serikali imekuwa ikiweka mifumo rahisi kwa wafanyabiashara na kitendo cha wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kutaibua tija kubwa kwa ustawi wa wafanyabiashara na taifa kiujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya PMM Group,Dkt Judith Mhina SPENDI ,amesema ujio wa ujumbe huo kutoka Oman wenye nia ya mashirikiano ya kibiashara kati ya Oman na Tanzania ni fursa kubwa na itasaidia kukuza uchumi kampuni yake na nchi kwa ujumla
Sambamba na hilo dkt Judith Mhina amesema kuwa PMM group imefarijika na ujio wa fursa hiyo ya kibiashara ambapo itawawezesha wafanyabiashara kuagiza biadhaa zenye uhitaji nchini ikiwemo bidhaa ya salfa pamoja na zile za ujenzi.
Aidha, Judith mhina amesema kuwa serikali imekuwa ikiweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hivyo ujio wa ujumbe huwo ni moja ya kutekelezwa kwa sera na mifumo bora katika kuwasaidia na kuwahudumia wafanyabiashara nchini.
Pia, ameiomba serikali kuendelea kutunga sera nzuri zitakazosaidia kuongeza idadi ya wafanyabiashara nchini ili kuongeza kasi ya ukuaji wa wafanyabiashara wakubwa watakaosaidia kuongeza kasi katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akizungumza kwa niaba ya uwakilishi wa ujumbe kutoka Oman, Mkuu wa Msafara kutoka Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) Oman, Salim Albusaid amesema ziara ya ujumbe huo nchini Tanzania ni kutambua fursa zilizopo nchini pamoja na kubadilisha fursa kupitia serikali hizo ikiwa pamoja na kudumisha mashirikiano ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.








