Wananchi 1182 Wajitokeza Kupima Maambukizi ya Ukimwi Wilaya ya Musoma

GEORGE MARATO TV
0


 Na Ada Ouko, Musoma.

WANANCHI 6 sawa na asilimia 0.5 kati ya wananchi 1182 waliopima virusi vya ukimwi (VVU) wakati wa mkesha wa mbio za Mwenge wa uhuru wilayani Musoma mkoani Mara wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Hayo yamebainishwa Agosti 18, 2025 na mkuu wa wilaya hiyo Juma Chikoka wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wilayani hapa alisema idadi hiyo ni sawa na wanaume 820 na wanawake 362 na kwamba walibainika na VVU wameunganishwa na huduma ya matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo(CTC).

" Idadi ya waliopima malaria ni wananchi 456 (wanaume ni 256 na wanawake ni 200) waliogundulika kuwa na vimelea vya malaria ni wananchi 22( wanaume 13 na wanawake 9) sawa na asilimia 4.8 na wote walipatiwa matibabu" alisema CHikoka.

Amesema jumla ya wananchi 112 walijitokeza kuchangia damu salama na kwamba wananchi 83 ndio waliokuwa wamekidhi vigezo vya kutoa damu hiyo na kusababisha kupatikana kwa chupa 83 za damu salama.

Amesema katika unasihi na upimaji ya hali ya lishe wilayani hapa wanaume 225 na wanawake 245 walipimwa hali ya lishe huku waliobainika kuwa na changamoto za lishe(uzito pungufu na uliozidi) walikuwa ni 137( wanaume 73 na wanawake 64) sawa na asilimia 29.14 ambapo wote walipatiwa unasihi.

Aidha amesema jumla ya wateja 142(wanaume 45 na wanawake 97) walijitokeza na kupewa huduma za uzazi wa mpango sambamba na ushauri wa kiafya.


KATIKA HATUA NYINGINE...

Dc Chikoka amesema Mwenge wa uhuru ulipokelewa kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda Agosti 16,2025 katika kijiji cha Kabulabula Kata ya Bugoji. 

Anaeleza kuwa Mwenge huo ukiwa katika Wilaya ya Musoma ulikimbizwa kwa umbali wa kilomita 160.9 na ulipita katika kata 11 za Manispaa ya Musoma ambazo ni Buhare, Mwisenge, Makoko,Mwigobero, Kitaji, Nyasho, Nyakato,Bweri, Mshikamano na Nyamatare.

"Katika mbio zake Mwenge wa uhuru umefanikiwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi, ulizindua mradi mmoja na kuweka jiwe la msingi miradi 2, kufungua mradi 1, kutembelea na kuona miradi 4, Ambapo miradi yote 8 ina thamani ya TSH 3,591, 239,074.93" aliongeza kusema Dc Chikoka.

Chikoka amesema katika Halmashauri ya wilaya ya Musoma Mwenge ulipita katika kata 10 ambazo ni Bugoji, Nyamboni, Bugwema, Suguti, Busambala, Mugango, Kiriba, Ifulifu, Nyakatende na Nyegina. Na kwamba Mwenge huo ulipita katika miradi 7 yenye thamani ya TSH 2,562, 794, 529.08 huku miradi 4 ilizinduliwa na miradi 3 iliwekewa jiwe la msingi.


























Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top