Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Mara Ndugu Ismail Ali Ussi leo amewasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61 tangu ulipoanza kukimbizwa hapa nchini mwaka 1964.
Akiwa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru, Ndugu Ussi akiongozwa na wanafamilia na wazee wa kimila, Ndugu Ussi ametembelea pia kaburi la Baba wa Taifa na kupata historia ya familia ya Mwalimu Nyerere.
Ukiwa nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwenge wa Uhuru umepokelewa na Chifu Japhet Wanzagi, kiongozi wa familia ya Mwalimu Nyerere na Chifu wa Kabila la Wazanaki.
Mbali na wanafamilia wa Mwalimu Nyerere, Viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi wameshiriki tukio hilo la kihistoria.








