kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru apongeza Mkakati wa Kupunguza Msongamano darasani wilayani Misungwi

GEORGE MARATO TV
0


 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Isamil Ali Ussi amezindua vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Jitihada wilayani misungwi mkoani mwanza.

Vyumba hivyo viwili vimejengwa kupitia shilingi millioni 50 za mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya misungwi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Ussi ameeleza kufurahishwa kwake na mpango mkakati wa halmashauri ya wilaya misungwi wa kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.

Ussi amesema kuwa mkakati huo utasaidia kuinua ari ya ujifunzaji na ufundishaji na hivyo kuongeza kiwango cha ufaulu.

Naye mkuu wa wilaya misungwi Johari Samizi amesema kuwa ujenzi wa madarasa hayo ulianzishwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuhakikisha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2026 wanapata nafasi.

Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani misungwi umeweka Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya majengo yenye urefu wa nusu kilometa kwa kiwango cha lami nyepesi unaogharamiwa kupitia fedha za tozo ya mafuta na unatekelezwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini(Tarura)kwa gharama ya shilingi millioni 411.

Pia umezindua huduma za afya na vifaa tiba vya kisasa kwenye zahanati ya nyamikoma ambavyo vitawezesha wananchi kupata matibabu ya uhakika sanjari na kuwaondolea wananchi adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa tano kufuata huduma za afya. 







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top