Rais Museveni Aagiza Kufukuzwa Kazi wafanyakazi 152 wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe

GEORGE MARATO TV
0

Rais wa Uganda Jenerali Mstaafu Yoweri Kaguta Museveni ameagiza Mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo(UCAA)kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi 152 walioajiriwa na Mamlaka hiyo bila kuwa na sifa stahiki.

Kwa mujibu wa Rais Museveni, wafanyakazi wanaotakiwa kufukuzwa walipata ajira kupitia Rushwa na hivyo kuchangia kuwepo kwa huduma duni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe. 

"Nimepokea Taarifa kuhusu Kushamiri kwa Rushwa katika Mamlaka ya UCAA ikiwemo Utoaji wa ajira kwa watu wasio na sifa na Matokeo yake kusababisha matatizo ambayo hayapaswi kuachwa kuendelea,Miongoni mwa matukio ya aibu na Fedheha ni kukwama kwa Mama Maria Nyerere katika lifti ya Uwanja wa Ndege wa Entebbe kwa muda wa dakika nne,Uchunguzi umefanyika na kubaini wafanyakazi 152 hawana sifa ambapo Naamuru wote wafukuzwe pamoja na wale wote waliowaajiri na nahitaji hilo litekelezwe kwa haraka sana"Rais Museveni alieleza katika Barua yake kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda Jenerali Edward Katumba Wamala.

Nakala ya Barua hiyo pia imetumwa kwa Makamu wa Rais Kapten Mstaafu Jessica Alupo,Waziri Mkuu Rhobinah Nabhanja na Waziri wa Elimu na Michezo Janet Museveni Miongoni mwa Viongozi wengine. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top