Spika wa BWZ ataka Watanzania kuwaunga mkono viongozi kudumisha Muungano

GEORGE MARATO TV
0

 


Na MASHAKA MHANDO, Tanga 

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BWZ) Zubeir Ali Maulid amewataka Watanzania kuwaunga mkono viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili waendeleze misingi imara ya Muungano.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika sherehe ya Muungano mkoani Tanga iliyofanyika Jijini Tanga, Spika alisema moja ya mambo yaliyosabanisha Muungano udumu ni viongozi kufuata misingi na malengo yaliyokusudiwa wakati wa kuasisiwa Muungano huo.

"Kwakuwa tupo katika kilele cha Muungano wetu, kuna baadhi ya mambo ya msingi yaliyosabababisha Muungano huu udumu, ni dhamira ya dhati ya viongozi wetu kusimamia misingi na malengo ya kuasisiwa kwake, hivyo tuwaunge mkono viongozi wetu wa Pande mbili za Muungano," alisema Spika huyo ambaye amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani hapa.

Aliwaasa kamwe wasiwaunge mkono watu wanaoleta chokochoko za kuvunja Muungano badala yake waendelee kuwa na Umoja na mshikamano kwa pande zote mbili.

Spika ambaye pia aligawa mitungi ya gesi 61 kwa wajasiriamali wadogo Jijini Tanga, alitaja faida sita zilizopatikana kutokana na Muungano huo akieleza kuwa ni pamoja na mshikamano wa kujengwa Taifa lenye kuongea lugha moja.

Alisema kuendelea kuimarika kwa ulinzi na Usalama wananchi kufanya shughuli zao bila kikwazo, matumizi ya sarafu moja yameimarisha uchumi kwa wananchi.

"Suala la Elimu mwanafunzi anasoma bila kujali anatokea upande gani wa Muungano lakini pia kuimarika kwa usafiri bila kutumia hati ya kusafiria na muingiliano wa mahusiano ya kijamii katika masuala ya ndoa.

Alisema kutoka na faida hizo Watanzania wanatakiwa kuuenzi Muungano na wafurahie matunda ya Amani na utulivu iliyopo nchini lakini pia kuwaunga mkono viongozi.

Awali mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Ustadh Rajabu Abdallah alisema wajibu wetu Watanzania ni kuwaenzi kwa wivu mkubwa waasisi wa Taifa hili kwa kuwa walitumia busara na hekima kuziunganisha nchi hizi mbili.


Alisema watu wanaobeza Muungano hawajui faida kubwa iliyopatikana hivyo akasisitiza ni vema wakawaenzi kutokana na fikra za kuanzisha nchi hii.

"Tuwashangae wanaotaka Muungano uvunjike Mimi nawafananisha na mdudu 'Tuta' Kombamwiko," alisema mwenyekiti huyo.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Salha Burian alisema wakati mkoa huo ukisherehekea sherehe ya Muungano, bado wana deni kubwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye wamepanga kumpa kura ifikapo Oktoba mwaka huu.

Mkuu wa mkoa alisema mkoa wa Tanga baada ya kuongoza katika zoezi la kujiandikisha nchini wamejipanga hasa vijana kuongoza kwa kura nyingi za kumchagua Rais kutokana na kazi kubwa alizofanya mkoani humo.

Alisema kazi alizofanya Rais za kuzindua miradi February mwaka huu alipofanya ziara mkoani humo hazina kifani na hivyo akataka wananchi wamuombee Rais.

"Rais alikuja hapa mkoani kwetu mwezi February ametuzindulia miradi mingi, hatuna deni naye na tunamuombea kwa mungu," alisema








Mwisho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top