Serikali ya Rais Samia kinara utoaji wa fedha za ruzuku kwenye kilimo - Waziri Bashe.

GEORGE MARATO TV
0

 


Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Hussein Bashe ameitaja Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kama serikali kinara kwa ukanda wa kusini mwa Afrika kwa kutoa fedha nyingi za ruzuku kwenye sekta ya kilimo cha mazao mbalimbali ya kibiashara.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Benki ya Taifa ya Ushirika leo Jumatatu Aprili 28, 2025 Jijini Dodoma, Waziri Bashe ametaja kuwa serikali ya Rais Samia kwa mwaka 2024/25 pekee imetoa ruzuku ya takribani Shilingi bilioni 99.5 kwenye zao la Pamba, sambamba na Bilioni nyingine 21 zilizotolewa kwenye zao la tumbaku kwa mwaka 2024/2025

Aidha Serikali ya Rais Samia pia kwa mwaka wa fedha 2024/25 imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 281 kwaajili ya pembejeo na miche ambayo wakulima wamekuwa wakipewa bure suala ambalo limewezesha sekta ya Korosho kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi wa tani 520,000 ambazo hazikuwahi kufikiwa tangu kupatikana kwa uhuru suala ambalo limewezesha wakulima kuuza mazao ya shilingi 1.8 kwa mwaka 2024/25 matarajio yakiwa kufikia Shilingi Trilioni 1.8 mpaka 1.9 kwa mwaka huu wa fedha wa serikali.

Bashe amezungumzia pia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita kwenye ruzuku ya Mbolea ambapo kwa mwaka 2021 wakati Rais anahutubia Bunge matumizi ya Mbolea yalikuwa tani 360,000 na kufikia 2023/24 matumizi hayo yamepanda na kufikia tani 860,000, huku mwaka huu wa fedha 2024/25 matumizi ya Mbolea yakitarajiwa kufikia Tani 1,200,000 ambapo jumla ya Bilioni 653 zimeshatolewa kama ruzuku ya Mbolea kwa miaka mitatu iliyopita.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top