Rais Samia Ameleta Mabadiliko Makubwa Kimaendeleo Nchini,Ikiwemo na Tarime-wasira

GEORGE MARATO TV
0


 Tarime.

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan serikali imeleta mabadiliko makubwa nchini ikiwemo wilayani Tarime ambako imejenga madarasa bila ya kuwachangisha wananchi kama ambavyo ilikuwa ikifanyika awali.

Wasira ameyasema hayo mjini Tarime leo Jumamosi Februari 8,2025 alipokuwa akizungumza na wanachama na wa chama hicho.

Amesema chama chake kimedhamiria kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi kwa kuendelea kuwatoa katika hali duni na kuwajengea misingi ya maisha bora kwa kadiri inavyowezekana huku akiwaomba wananchi kuendela kukiamini na kukipa nafasi ya kuendelea kushika dola na kuwatumikia.

“Tunaendelea kufanya mapinduzi ya maisha ya watu na ndiyo maana watu wa Tarime sasa ni watu tofauti na waliokuwepo miaka 60 iliyopita nawashangaa wanoasimama na kunasema hatujafanya kitu, tumefanya, tumesomesha watu wengi sana hata wanaosema hatujafanya chochote tumewasomesha na kuwapa uhuru wa kusema hatujafanya chochote," amesema 

Amesema katika kipindi cha miaka 60 iliyopita chama hicho kimefanya mambo makubwa ya kimaendeleo hali iliyopelekea kuimarika kwa maisha katika sekta mbali ikiwemo ya elimu na huduma za jamii kwa ujumla.

Amesema kutokana na ukweli kuwa chama hicho kilianzishwa kwa nia ya kuwaokomboa na kuwaletea maendeleo wananchi jukumu hilo bado ni la msingi kwa chama hicho hivyo wananchi wanapswa kuendelea kukiamini na kukipa ridhaa ya kushika dola ili kiweze kuwatumikia.

"Wako wengine wanasema miaka 60 eti hatujafanya kitu, naomba muwasamehe kwa kuwa hawajui wanachosema, kwa sababu mimi kwa umri wangu nilikuwepo niliijua Tarime kabla ya uhuru na nawaona wapo wazee hapa pia waliijua," amesema 

Huku akitupa vijembe kwa vyama alivyodai vyenyewe ni vya matusi na ugomvi, amewataka wananchi kupuuza maneno ya watu akidai hata sekta ya afya imeimarika ikilinganishwa ilivyokuwa miaka 60 iliyopita.

“Juzijuzi wamefanya mkutano wao Dar es Salaam pale wamegawana fito, mmoja kaenda na wake na mwingine kaenda na wake, kuna chama hapo? Sasa wanakuja kukwambieni Tarime muwapigie kura wamefanya kitu gani, maana mtu hupigi kura bila ya sababu,” ameongeza

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara,Evans Mtambi amemuomba Wasira kusaidia katika kuhakikisha uwanja wa Ndege wa Musoma unakamilika ikiwa pamoja na uwanja wa Ndege wa Serengeti.

Uwanja wa ndege wa Musoma unajengwa na kukarabatiwa kwa gharama ya zaidi ya Sh35 bilioni ambapo hivi karibuni ujenzi wake ulisimama kutokana na ukosefu wa fedha 

Mtambi amesema Mkoa wa Mara umeendelea kuwa na amani jambo ambalo limekuwa rafiki kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na kwamba miundombinu kama uwanja wa ndege ni moja ya vivutio vya uwekezaji na wawekezaji kwa ujumla.

"Ili mkoa uweze kunufaika na rasiliamli zilizopo ni lazima tuwe na wawekezaji wa kutosha hivyo miundombinu kamauwa ja wa ndege ni moja ya kichocheo cha wawekezaji, tunakuomna Makamu Mwananchi usaidie kuhakikisha hili linakamilika," amesema Mtambi

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime, Marwa Ngicho amesema wana CCM wanapaswa kuvumuliana na siyo kuvuana nguo wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, 2025.

Amesema wilaya hiyo yeye majimbo mawili imejipanga kushinda kata zote upande wa Madiwani pamoja na Wabunge.

Nao, Wabunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki na Tarime Vijijini, Mwita Weitara wamepongeza Serikali kwa kupeleka miradi ambayo imetatua kero za wananchi ukiwemo wa ujenzi wa Soko la kisasa na miradi ya maji.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top