Waziri Mhagama:Tanzania inakuja na Mifumo imara ya Bima ya afya kwa Wote Nchini

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagamana na ujumbe wake akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Ismail Rumatila, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu  pamoja na wataalam wengine Desemba 09, 2024 wamefanya ziara ya mafunzo ya jinsi mfumo wa uendeshaji wa masuala ya afya unavyofanya kazi chini ya Wizara ya Afya Uingereza.

Hatua hii ni muhimu kuelekea utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote nchini Tanzania kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na mifumo imara katika usimamiaji wa huduma za afya.

"Miongoni mwa mambo tuliyojifunza kutoka kwa wenzetu wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Afya ya Uingereza Dkt. Kevin Miles ni pamoja na jinsi huduma za afya kupitia Bima ya Afya zinavyotolewa kwa wanachama, mifumo ya utoaji wa huduma kupitia Bima ya Afya jinsi inavyofanya kazi pamoja na namna ambavyo wanalipwa watoa huduma hao," amesema Waziri Mhagama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top