REA Kutoa Majiko ya Gesi Yenye Ruzuku Kwa Wananchi Nchini Nzima

GEORGE MARATO TV
0



Na Angela Sebastian-Bukoba 

MENEJA mradi wa Nishati safi kutoka wakala wa Nishati vijijini (REA)
Mhandisi Deusdedit Malulu amesema wanatarajia kutoa majiko laki 452 nchi nzima yenye thamani ya shilingi bilioni 8.6 yatakayouzwa kwa wananchi kwa gharama nafuu ya shilingi elfu 17,500 tu.

Kwa mujibu wa Mhandisi Malulu, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa majiko hayo yenye ruzuku kutoka Serikalini lengo likiwa ni kila mwananchi kutumia nishati safi wakati wa kupika, kuepuka uharibifu wa misitu, kwa kuchoma mkaa,kuni na kuepuka uharibifu wa mazingira.

Amesema kwa mkoa wa Kagera wanatarajia kunufaika kwa kupatiwa majiko ya kupikia yenye ruzuku ambapo jumla ya majiko ya gesi ya kilo sita yapatayo 22,785 yenye thamani ya shilingi milioni 398 yatatolewa na sharti la kupata jiko ni kuwa na namba au kitambulisho cha NIDA ili kuwezesha kuwafikia wananchi wote.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa huo  Stephen Ndaki ameomba uongozi wa REA nchini kabla ya kuanza kuuza mitungi hiyo ambayo itauzwa kupitia kwa mawakala waliowachagua kila mkoa ,ni vizuri wananchi wakapatiwa mafunzo kuhusu umuhimu wa majiko hayo ya ruzuku   na matumizi yake kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top