Rais Samia;daraja la Jp Magufuli kuanza kutumika februari mwaka 2025

GEORGE MARATO TV
0



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan,amekagua Maendeleo ya ujenzi wa daraja la kimkakati la Jp Magufuli linalojengwa ndani ya ziwa Victoria litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza na kusema ameridhishwa na ujenzi huo.

Rais Samia amesema kuwa Ujenzi wa daraja la Jp Magufuli unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi billioni Mia Saba umefikia asilimia 93.

Akizungumza na wakazi wa kigongo wilayani Misungwi,Rais Samia amesema kuwa daraja hilo lenye urefu wa kilometa tatu pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 litafunguliwa februari mwakani. 

Daraja la Jp Magufuli ni la kwanza kwa urefu katika nchi za afrika mashariki na kati na litakuwa kiungo muhimu cha usafiri na usafirishaji baina ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mataifa Jirani ikiwemo UGANDA,BURUNDI,RWANDA na JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

Daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba Tani 120 za Mizigo na linatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo februari mwakani.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amezungumzia maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa ya SGR kipande cha tano kutoka Mwanza Hadi Isaka mkoani shinyanga ambao amesema Umefikia asilimia 60.

Samia amesema serikali imedhamiria kukamilisha ujenzi wa kipande hicho cha Reli na kukiunganisha na vipande vya Isaka-Tabora na Tabora-Makutopora ambavyo viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi. 

Amebainisha kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutarahisisha uchukuzi wa abiria na mizigo pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top